By Perez Karisa, June 25, 2026
Mshumaa wa kumbukumbu umeendelea kuwashwa na Wakenya kote nchini kama ishara ya mwanga, amani na matumaini, huku taifa likikumbuka vijana waliopoteza maisha yao katika maandamano ya Juni 25, 2024.
Siku hii ya kumbukumbu imebeba hisia nzito kwa familia nyingi ambazo bado zinakabiliwa na maumivu ya kupoteza wapendwa wao kwenye maandamano ya juni mwaka jana wakiandamana kwa ajili ya maslahi yao ya kiuchumi.

